14 Agosti 2025 - 13:29
Arubaini: Jukwaa la Haki, Amani na Uadilifu, na ni Taa ya Uongofu na Jahazi la Uokovu

Historia inaonyesha kuwa jukwaa hili lina mizizi imara katika imani, haki na uadilifu. Lilianza na mtu mmoja au wawili zaidi ya karne kumi zilizopita. Pamoja na changamoto nyingi zilizowakumba waliolipanda, idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila mwaka - hasa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa hakika, ulimwenguni kumekuwepo majukwaa makubwa ya mikusanyiko - yawe ya kidini, kisiasa, kitamaduni, michezo au burudani. Hata hivyo, jukwaa la Arubaini (40) ya Imam Hussein (as) ni tofauti kabisa na majukwaa mengine.

Asili na Mizizi ya Jukwaa la Arubaini

Historia inaonyesha kuwa jukwaa hili lina mizizi imara katika imani, haki na uadilifu. Lilianza na mtu mmoja au wawili zaidi ya karne kumi zilizopita. Pamoja na changamoto nyingi zilizowakumba waliolipanda, idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila mwaka—hasa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Upekee wa Jukwaa Hili
Ni jukwaa lenye lugha ya kivitendo na dhihirisho halisi la mapambano ya maumbile ya mwanadamu kupenda haki, ukweli na uadilifu.
Limekuwa ni jukwaa la kila aliyekata tamaa na mifumo mibovu ya uendeshaji wa mambo, ukandamizaji, ukoloni wa kunufaisha wachache, na hali ya kudhoofika kwa maadili ya kijamii.
Kila anayechoshwa na hali hiyo hupenda kulipanda na kuungana na wenzake wanaodai haki na uadilifu.

Kiini cha Harakati
Kiini cha jukwaa hili ni yule aliyejitolea kila kitu chake ili kurejesha amani ya kweli, uadilifu halisi, usawa na haki; na kukata minyororo ya utumwa na unyonge.
Yeye si mwingine bali ni mjukuu wa Mkombozi wa Waarabu waliokuwa katika ujahilia-Mtume wa huruma, mkweli na muaminifu Muhammad (s.a.w.w.)-Imam Hussein (a.s.).

Kauli Mashuhuri:  “Hakika Hussein -as- ni Taa ya uongofu na ni Jahazi la uokovu.”

Mwisho kabisa tuna malizia Makala yetu kwa maneno haya Muhimu:
Labayka ya Hussein! Labayka ya Hussein! Labayka ya Hussein!

Imetolewa na:
Jukwaa la Hussainiyya ya Moa, Tanga - Tanzania.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha